Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Tuesday, July 31, 2012

JLO ASHEREHEKEA BIRTHDAY YAKE KATIKA BOAT NA KING'ASTI WAKE.

Perfect dress with perfect shoes
KEKI IKISAFIRISHWA KWENDA KATIKA BOAT.



Monday, July 30, 2012

KIDUNDWA ADUNDWA OLIMPIKI

Bondia wa Tanzania, Selemani Kidunda (kulia) akiwa hoi baada ya kudundwa kirahisi kwa pointi 20-7 dhidi ya bondia wa Moldova, Vasilii Belous katika pambano la uzito wa welter (69kg) mzunguko wa 32 kwenye Ukumbi wa ExCeL katika michuano ya Olimpiki ya London 2012 leo Julai 29, 2012.
Bondia wa Tanzania, Selemani Kidunda (kushoto) akishambuliwa na bondia wa Moldova, Vasilii Belous wakati wa pambano lao la uzito wa welter (69kg) mzunguko wa 32 kwenye Ukumbi wa ExCeL katika michuano ya Olimpiki ya London 2012 leo Julai 29, 2012.
Bondia wa Tanzania, Selemani Kidunda (kushoto) akiendelea kuadhibiwa na bondia wa Moldova, Vasilii Belous wakati wa pambano lao la uzito wa welter (69kg) mzunguko wa 32 kwenye Ukumbi wa ExCeL katika michuano ya Olimpiki ya London 2012 leo Julai 29, 2012.

Friday, July 27, 2012

JOHN KOMBA AREJEA NYUMBANI BADA YA KUFANYIWA UPASUAJI INDIA


Mkurugenzi wa  Tanzania One Thetre (TOT) ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba akizunguma na waandishi wa habari nyumbani kwake, Mbezi Tangi Bovu, Kawe, Dar es Salaam, leo  wakati akizungumzia hali ya afya yake baada ya kurejea nchini akitoka nchini India alikokwenda kufanyiwa upasuaji. Kushoto ni Mkewe, Salome Andrew Komba. 
**********************************
NA BASHIR NKOROMO

MKURUGENZI wa Kundi la Tanzania One Theatre (TOT) ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba amerejea kutoka India ambako amefanyiwa upasuaji kumtibu ugonjwa wa nyonga ulilokuwa ukimsumbua upande wa mguu wake wa kulia.

Akizungumza na waandishi wa habari, jana Julai 27, 2012, nyumbani kwake Mbezi kwa Komba, mjini Dar es Salaam, Komba alisema amerejea nchini,  Juzi,  baada ya kupatiwa matibabu hayo kwenye hospitali ya Appolo iliyopo Hydrabad nchini India tangu mwanzoni mwa wezi huu.

Alisema, aliondoka nchini, Julai 2, 2012, baada ya kupelekwa na serikali kwa maelekezo ya Rais Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge Anna Makinda na Katibu wa Bunge John Kashilila na kwamba alikwenda baada ya kukosa matibabu hapa nchini kwa sababu ya mgomo wa madaktari.

"Siku napelekwa Muhimbili tu, tayari madaktari walikuwa wameanza siku ya kwanza ya mgomo wao, nikawa sina namna ila kuujulisha uongozi wa Bunge na kisha nikamuomba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, naye kwa mamlaka yake akanisaidia haraka kama ambavyo huwasaidia wengine kwenda kutibiwa nje", alisema Komba.

Alisema, uzito ulichangia sana kusababisha mifupa kusagana kwenye nyonga upande wa mguu wa kulia, ambapo hadi anakwenda India alikuwa na uzindo wa kilo 138 wakati wastani wa uzito aliotakuwa kuwa nao kulingana na ukumbwa wa mwili wake ni kilo 90 au 100 tu.

"Amesema, baada ya matibabu amerejea nchini akiwa na uzito wa kilo 128 ambao hata hivyo ametakiwa kuudhibiti na kuupunguza katika siku hizi ambazo atalazimika kupumzika nyumbani kabla ya kuanza kazi, Mwezi Septemba mwaka huu kama alivyoelekezwa na madaktari.

Akizungumzia upasuaji ulivyoendeshwa, Komba alisema, ulichukua saa tano na kukamilika bila matatizo katika upasuaji huo ambao alisema sehemu iliyopasuliwa ni ya ukumbwa wa futi moja.

Alisema, hata hivyo baada ya upasuaji huo, hakuweza kurejea katika wodi ya kawaida, kwa sababu majongwa kadhaa yaliibuka ikiwemo homa kali, presha, hivyo akalazimika kulazwa katika wodi ya wagonjwa waliopo kwenye uangalizi maalum (ICU) kwa siku tano.

"Sasa nimerejea nikiwa mzima, kwa sasa natumia fimbo hii, ili kuwezesha uzito uzilemee upande wa kulia nilikopanyiwa upasuaji, lakini sijambo kabisa", alisema Komba.

Komba alilaani baadhi ya vyombo vya habari ambavyo viliripoti kwamba katika kuugua kwake alikuwa mahututi na kwamba alikuwa anaugua figo.

"Jamani ninyi waandishi wa habari, jizoesheni kuandika habari zilizokamilika siyo kurashia-rashia tu na kuzusha uongo, mfano gazeti moja liliandika eti naugua figo nipo mahututi, wakati si kweli kabisa, ilikuwa jambo rahisi tu, kuja hapa nyumbani na kuniuliza au kuuliza mke wangu lingepata kwa uhakika ninachoumwa", alisema Komba.

Wednesday, July 25, 2012

MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA LEO



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, wakati alipowasili kwenye uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Julai 25, 2012 kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo, Julai 25, 2012 kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, leo

Kutoka (kushoto) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho, ........ na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, wakiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakihudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, leo Julai 25, 2012.

Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akiweka Ngao na Mkuki kwenye Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam



Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Julai 25, 2012.

Tuesday, July 24, 2012

BASI LA SIMBA MTOTO NA DAR EXPRESS YAGONGANA USO KWA USO ENEO LA WAMI

 Hali ndivyo ilivyokuwa...
 Abiria wakiwashusha wenzao.
Basi la Dar Express lililokuwa linatoka Arusha na basi la Simba Mtoto lililokuwa linaenda Tanga yamegongana uso kwa uso maeneo ya Wami. Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa k
atika hospitali ya Chalinze. 
Mmoja kati ya abiria waliokuwamo katika mabasi hayo akiwa amejeruhiwa usoni baada ya ajali hiyo. Picha na Mtaa kwa Mtaa Blog.

WAZIRI EAMAWASILIANO WAMIUNDOMBINU ZANZIBAR

Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu wa Zanzibar, Hamad Masoud (pichani) amejiuzulu kufuatia shinikizo za za watu na maandamano.
Kumekuwa na msukumo kutoka kwa makundi mbali mbali ya kutaka waziri huyo ang'atuke kufuatia kuongezeka kwa ajali za baharini kati Hatua hii imekuja kufuatia madai ya wananchi kuwa ajali za meli zimekuwa zikiongezeka mjini Zanzibar bila yeye kuchukua hatua yeyote.
Mbali na kujiuzulu kwa Hamad kama Waziri, Rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein ameunda Tume ya kuchunguza kiiina cha Meli hiyo ya MV Skagit kuzama na kuuwa watu.
Mwenyekiti wa tume hiyo atakuwa Jaji Abdulhakim Ameir Issa, wanachama watukiwa Meja Jenerali S.S. Omar, Komanda Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla Yussuf Jumbe, Kaptein Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq,Kaptein Hatibu Katandula, Bi. Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban Ramadhan Abdalla Katibu wa Tume.
Kufuatia shinikizo hizo Siku ya Ijumaa ,tarehe 20 Julai ,Hamad Masoud alimuandikia barua rais wa Zanzibar kumuomba kujiuzu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka chama tawala cha CCM, Rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud kujiuzulu.
Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Rais ,Dk Shein amemteua Mbunge wa Jimbo la Ziwani Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri mpya wa Miundombinu na Mawasiliano.
Taarifa kutoka ikulu zinasemna kuwa uteuzi wa Bwana Rashid Seif Suleimna utaanza mara moja

Sunday, July 22, 2012

BODI YA MISS UTAALII TAIFA YAFUTA MISS UTAALII KANDA YA ZIWA



BODI YA TAIFA YAFUTA MISS UTALII KANDA YA ZIWA 2012


Bodi ya Taifa ya Miss Tourism Tanzania Organisation (MTTO),imefuta na kutokulitambua shindano la Miss Utalii Kanda ya Ziwa 2012 lililo fanyika New Mwanza Hotel ,wakati taifa likiwa katika maombolezo ya msiba mkubwa wa kitaifa wa watu waliopoteza maisha katika ajali ya meli iliyo tokea Zanzibar.
Bodi imechukua hatua ya kulifuta na kutolitambua shindano hilo, ambalo limefanyika bila ya kuzingatia misingi ya kibinadamu na hata uzalendo kwa Taifa. Waandaaji wa shindano hilo Fania Hassan wa Fania Beauty Salon,pamoja na kutambua kuwa taifa lipo katika maombolezo ya siku tatu kwa tangazo na tamko la serikali, bado hakuzingatia maelekezo ya waandaaji wa Taifa ambao walisitisha mashindano ya Miss Utalii Tanzania katika ngazi zote,likiwemo lile la Miss Utalii Kinondoni 2012 ambalo lilikuwa lifanyike tarehe 20-7-2012 katika ukumbi wa Traveltine Dar es Salaam ambalo sasa litafanyika 31-7-2012 katika ukumbi wa Club Maisha Oyterbay na lile la Miss Utalii Ilala 2012 ambalo lilikuwa lifanyike 21 -7-2012 katika ukumbi wa Eriado View pont Pugu Dar es Salaam ambalo sasa lifanyika siku ya Iddy Pili katika ukumbi wa Eriado point View Pugu.
Bodi ya mashindano katiaka kikao chake cha dharula kilichofanyika leo asubuhi baada ya kupata taarifa kutoka kwa vyanzo vyetu vya uhakika,juu ya kufanyika kimyakimya kwa shindano hilo imeamua kuchukua hatua hiyo kali ya kulifuta na kutolitambua shindano hilo, ili iwe fundisho kwa waandaaji wengine wasiozingatia maagizo kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mashindano haya. 
Bodi imesikitishwa sana na tukio hilo kisilo la kizalendo, na inawaomba radhi watanzania wote,ndugu na jamaa wote waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo,serikali, mamlaka zote za mkoa wa Mwanza, mamlaka za sanaa,wadhamini na wadau mbalimbali wa mashindano ya urembo utalii na utamaduni nchini na nje ya nchi.
Washiriki wote watalazimika kusubiri tarehe mpya ya kufanyika kwa shindano hilo,baada ya mfungo wa ramadhani,ambapo pia watagharamiwa gharama zote za ushiriki wao upya,kama kanuni na taratibu za mashindano zinavyo bainisha kuwa washiriki wote wa mashindano ya Miss Utalii tanzania wanagharamiwa gharama zote za mavazi,usafiri,vinywaji,chakula na saluni.
Kamati ya nidhamu ya mashindano haya itakutana mwisho wa mwezi ili kujadili hatua zaidi za kuchukua dhidi ya waandaaji hao wa Miss Utalii kanda ya Ziwa 2012.
Haiwezekani hata kidogo wakati taifa lina omboleza halafu mtu anatumia mashindano haya ambayo ni alama ya urithi wa Taifa na kielelezo cha utamaduni wa mtanzania kukiuka utamaduni,mila na desturi za Tanzania,tena wakati hata serikali 
imetangaza maombolezo na bendera zinapepea nusu mlingoti. 
Kwa mara nyingine tena tunaungana na watanzania wote kuwapa pole Ndugu zetu wa Zanzibar walio Potelewa na ndugu jamaa pamoja na Marafiki, Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape Nguvu katika kipindi hiki kigumu. Pia kwa wale majeruhi na ambao wapo kwa matibabu pia Tunawaombea wapate kupona Haraka ili warejee katika kazi zao za kujenga taifa. 
Miss Utalii Tanzania ni Alama ya Urithi wa Taifa – Utalii ni Maisha ,Utamaduni ni Uhai wa Taifa.
Asante,
Abubakari Omary Bakari
MKURUGENZI WA UTAWALA NA FEDHA - MISS TOURISM TANZANIA ORGANISATION

Saturday, July 21, 2012

SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI ANNE MAKINDA ATOA POLE KWA RAIS WA ZANZIBAR

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, aliyeongozana na Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri, walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kutoa  pole kwa Rais, kutokana na msiba wa ajali ya Meli ya Mv Skagit ya Kampuni ya Segull iliyozana juzi wakati Ikitokea Dar es Salam, kuelekea  Zanzibar. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama, Cynthia Hilda Ngoya, akiwa katika  ujumbe wa Wabunge  walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kutoa  pole kwa Rais.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Margareth Sitta, ambaye pia ni mmoja kati ya Wajumbe wa bunge la Jamhuri waliofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kutoa  pole kwa Rais.

Friday, July 20, 2012

HAYA SASA, WALE WALIOTAMANI KUMUONA MTOTO WA BEYONCE TOKA AKUE… NDIO HUYU.

Hizi picha zimepigwa na mtu tu ambae alishtukia Beyounce na mwanae wakifanya shopping mbele yake, akazipiga na kutweet… Blue Ivy kakua.
Ni miezi kadhaa toka mara ya mwisho dunia ilipomuona Blue Ivy kwa uwazi kiasi hiki.
Hizi ni picha ambazo zilitolewa bure na Beyonce na Jay Z miezi kadhaa iliyopita zikimuonyesha mtoto wao ambae wengi tulidhani wangeuza kwa mamilioni ya dola picha za mtoto wao kama walivyofanya mastaa wengine ikiwemo J.Lo!

Wednesday, July 18, 2012

MATUKIO YA AJALI YA KUZAMA KWA BOTI YA SEAGULL KATIKA PICHA

 Askari wa Jeshi wakibeba miili ya watu waliokufa katika ajali hiyo ya Boti ya Seagull ya kuzama Baharini, wakihifadhi katika Bandari ya Zanzibar.
 Sehemu ya wananchi waliojitokeza kushudia ajali hiyo na kuhakiki ndugu jamaa na marafiki, wakiwa katika Bandari ya Zanzibar.
 Miili ya waliokufa katika ajali hiyo, ikibebwa baada ya kuopolewa majini.
 Askari wakijipanga upokea maiti waliokuwa wakishushwa katika Boti za uokoaji.
 Wanahabari wakihojiana na mtoa taarifa.

JOYCE BALUHI NDIYE MISS MOROGORO 2012

Miss Morogoro 2012 Joyce Baluhi (katikati) akiwa na washindi wenzake, Salvina Kibona mshindi namba mbili (kushoto) na Irene Thomas mshindi namba tatu mara baada ya kumalizika kwa shindano la Miss Morogoro lililofanyika katika ukumbi wa  Morogoro Hoteli mwishoni mwa wiki.
Miss Moro Morogoro 2012 Joyce Baluhi kushoto akiwa na Miss Morogoro 20111, Asha Salehe kulia mara baada ya kumkabidhi taji hilo.
Mgeni rasmi shindano la Miss Morogoro 2012 ambaye ni Afisa Mwendeshaji wa mfuko wa pensheni kanda ya mashariki na kati (PPF) Astronaut Liganga kulia liyesimama akiwa katika picha ya pamoja na Miss Morogoro 2012, Joyce Baluhi aliyekaa, Mratibu wa shindano hilo Frank Kikambako kushoto aliyesimama na warembo wengine walioingia tano bora mara baada ya kutangazwa matokeo na kuwapata washindi.
Hawa ndiyo warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bara kutoka na kuchujwa kupata mshindi wa kwanza, pili na tatu ambao warembo hao watashiriki shindano la Miss Kanda ya Mashariki.
  Picha ya pamoja ya washiriki wote 13 ambao walishiriki shindano hilo baada ya kupanda kujukwaani na vazi la ubunifu, ufukweni na jioni katika kinyang'anyiro hicho.
  mrembu naye akiwa katika vazi la ubunifu.
 
Mrembo Prisca Mengi (18) akipita mbele ya majaji na mashaki na vazi la ubunifu.
Rais wa bende ya FM Academia (wazee wa Ngwasuma), Nyoshi El- Saadat akiimba wakati bende yake ikitumbuiza mashabiki waliohudhuria shindano hilo ndani ya viwanja vya wazi vya hoteli ya Morogoro.
Mmoja wa wanenguaji wa bendi ya FM Adademia akicheza kwa aina mpya kwa staili ya Vundesa.

JOYCE Baluhi (22) ameibuka katika shindano la kumsaka Miss Morogoro 2012 baada ya kutwaa taji hilo lililokuwa na ushindani wa hali ya juu lililofanyika kwenye viwanja vya wazi vya hoteli ya Morogoro mwishoni wa wiki mkoani hapa.
Shindano hilo ambalo lilishirikisha warembe 13 ambapo Salvina Kibona (20) kwa kutwaa nafasi ya pili wakati nafasi ya tatu ikichukuliwa na Irene Thomas (20) ambao walifanikiwa kuvuka katika hatua ya tano bora.
Dalili za Baluhi kutwaa kwa taji hilo zilionekana mapema hasa katika onyesho la vazi la ubunifu, ufukweni na jioni kabla ya kumalizia kizingiti cha mawaswali na kuibua shngwe na ndelemo kutoka kwa mashabiki waliohudhuria shindano hilo kwa kila hatua ambayo akionekana mlimbwende huyu baada ya kulitawala jukwaa.
Katika shindano hilo ambalo lilisindikizwa na bendi ya muziki wa dansi ya bende ya FM Academia (wazee wa Ngwasuma) chini ya Rais wao, Nyoshi El- Saadat lilikonga nyoyo za wapenzi wa dansi na shindano hilo ambapo walitumbuiza nyimbo mbalimbali zilizopo katika chati hivi sasa.
Mwandaaji wa shindano hilo la Miss Moro 2012, Frank Kikambako alisema kuwa mshindi wa kwanza amejipatia sh400,000 huku mshindi wa pili akipata sh300,000 na mshindi wa tatu akipata zawadi ya sh250,000 na washiriki wote walioshiriki shindano hilo wakiambulia pesa ya sh50,000 kila mmoja kama kifuta jasho.
Naye mgeni rasmi katika shindano hilo Afisa Mwendeshaji wa mfuko wa pensheni kanda ya mashariki na kati (PPF), Astronaut Liganga alisema kuwa warembo waliofanikiwa kuingia tano bora na hatimaye kumpata Miss Moro 2012 ambao wote watashiriki shindano la Miss Kanda ya Mashariki kuwa na nidhamu mzuri itayochangia na sifa nyingine kuvuka vikwazo katika shindano hilo.
Aliwataja warembo ambao walifanikiwa kutinga hatua ya tano bora ni Nafya Waziri (19) na Betina Lawurence (20).
Liganga alisema kuwa sifa pekee katika tasnia nyingi za michezo ikiwemo na urembo ni kuwa na nidhamu mzuri na kuwataka washiriki wengi ambao hawakupata nafasi ya kusonga mbele kuendeleza nidhamu walioionyesha katika kambi ya Miss Morogoro.

LISA AENDA CHINA KUSHIRIKI MISS WORLD 2012


 Miss World Tanzania 2012, Lisa Jensen akipunga mkono wakati akiondoka katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akieklekea nchini Nchina kushiriki shindano la Miss World 2012. Lisa anaiwakilisha Tanzania katika shindano hilo.
 Lisa akisikiliza jambo kutoka kwa Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandajai wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga(hayupo pichani).
 Lundenga akimsindikiza Lisa kwenda kukaguliwa tayari kwa safari ya nchini China.
   Lisa akiwaeleza jambo Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandajai wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kushoto) na Afisa Habari wa Kamati ya  Miss Tanzania, Hidan Rico
  Lisa akisikiliza jambo kutoka kwa Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandajai wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga
  Lisa akiwaeleza jambo Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandajai wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kushoto) na Mkuu wa Itifaki wa kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye.
Hashim Lundenga akisalimiana na mama mzazi wa Lisa Jensen wakati wa kumsindikiza mrembo huyo.